Habari hizo zimethibitishwa na familia yake na promota wa mieleka kutoka Mexico Lucha Libre AAA Worldwide.
Misterio Sr, aliyezaliwa Miguel Ángel López Díaz, alikuwa mtu mashuhuri katika eneo la lucha libre la Mexico, Alishindana katika mashirika mashuhuri ya mieleka ikiwa ni pamoja na Pro Wrestling Revolution, Tijuana Wrestling, na World Wrestling Association (WWA).
Mbali ya kuwa Mwanamieleka Misterio Sr. alijulikana kwa kuwashauri wacheza mieleka wengi, akiwemo mpwa wake, Rey Mysterio wa WWE, ambaye alikua bingwa wa dunia mara tatu. Misterio Sr. pia alifundisha nyota kama vile Konnan, Psicosis, Halloween, na Damian 666.
Chanzo cha kifo chake hakijawekwa wazi mara moja, lakini inakuja wiki chache baada ya kufariki kwa babake Rey Mysterio, Robert Gutierrez.